IQNA

Kongamano la Siku ya Kimataifa ya Quds nchini Senegal

13:02 - June 20, 2016
Habari ID: 3470401
Kongamano la Siku ya Kimataifa ya Quds limepangwa kufanyika katika Ijumaa y Mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mjini Dakar, Senegal kwa lengo la kuunga mkono harakati za ukombozi wa Palestina.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo lenye anuani ya "Changamoto za Kuleta Mshikamano wa Kuunga Mkono Palestina" limepangwa kufanyika tarehe Mosi Julai.

Kituo cha Utamaduni cha Iran mjini Dakar kitashirikiana na Kamati ya Kuunga Mkono Palestina Dakar katika kuandaa kongamano hilo. Kongamano hilo la SIku ya Kimataifa ya Quds litafanyika katika Kituo cha Kiislamu mjini Dakar.

Kila Ijumaa ya Mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hufanyika maandamano na makongamano kote duniani kuunga mkono mapamabano ya Wapalestina ambao wanapiga kuikomboa ardhi yao inayokaliwa na utawala wa Kizayuni wa Israel. Mijumuiko hiyo ya kuwaunga mkono Wapalestina huwaleta pamoja Waislamu na wasio kuwa Waislamu ambao mbali na kutangaza mshiakamano wao na Palestina pia hulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Mwaka huu Siku ya Kimataifa ya Quds itafanyika Julai Mosi.

/508491

captcha