IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Waislamu watajitokeza kwa wingi katika maandamano ya Siku ya Quds

8:59 - June 30, 2016
Habari ID: 3470424
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Waislamu kote duniani watajitokeza kwa wingi katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds kwa lengo la kuwaunga mkono Wapalestina wanaodhulimiwa.

Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alitoa kauli hiyo siku ya Jumatano mjini Tehran alipokutana na mkuu pamoja na maafisa wa ngazi za juu wa vyombo vya mahakama vya Iran. Kiongozi Muadhamu aliongeza kuwa: "Kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu, Ijumaa hii, kwa mara nyingine sauti ya kutetea watu madhulumu wa Palestina itasikika kote Iran na katika ulimwengu wa Kiislamu na Umma wa Kiislamu utatekeleza wajibu wake muhimu wa kutetea waliodhulumiwa."

Kwingineko katika hotuba yake, Kiongozi Muadhamu aliashiria hukumu ya mahakama ya Marekani ya kuchukua udhibiti wa mali za Iran kwa visingizio visivyo na ukweli wowote na madai yasiyo na msingi, Kiongozi Muadhamu ametaka haki za Iran zilizokiukwa zifuatiliwe kupitia vyombo vya mahakama za kimataifa.

Aidha ametaka vyombo vya mahakama Iran kufuatilia haki za maelfu ya waathirika wa ugaidi Iran kwa kuanzishwa kesi dhidi ya waliohusika na mauaji hayo ya kigaidi na waliounga mkono magaidi wazi wazi na kwa siri.

Hali kadhalika Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi amevishauri vyombo vya mahakama Iran kutetea shakhsia Waislamu waliodhulumiwa duniani.

Ayatullah Khamenei amesema kuhuisha haki za binadamu za Kiislamu katika uga wa kimataifa ni jukumu jingine la vyombo vya mahakama vya Iran. Ameongeza kuwa, haki za binadamu katika nchi za Magharibi zimejengeka katila msingi ghalati na hivyo kuna haja ya kuwabainishia walimwengu kuhusu haki za binadamu za Kiislamu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amelaani hatua ya Umoja wa Mataifa kufumbia macho mauaji ya watoto wa Yemen. Amesema hatua ya Umoja wa Mataifa kupokea pesa kutoka kwa baadhi ya nchi na hivyo kupuuza mauaji ya watoto wa Yemen ni jambo ambalo ni aibu kwa jamii ya mwanadamu. Amesema hii ni kashfa kubwa iliyo dhidi ya haki halisi za binadamu na kwamba jambo hili linapaswa kushughulikiwa katika vyombo vya mahakama kimataifa.

3511538

captcha