IQNA

UNESCO yapitisha azimio la kusisitiza Msikiti wa Al Aqsa ni milki ya Waislamu

14:57 - October 19, 2016
Habari ID: 3470620
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limethibitisha tena kwamba msikiti mtukufu wa Al-Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu ni milki ya Wapalestina.

Msemaji wa shirika hilo la Umoja wa Mataifa lenye makao makuu yake mjini Paris, Ufaransa amesema Bodi ya Utendaji ya shirika hilo ilipitisha rasmi Jumanne azimio lililopewa jina la "Palestina Inayokaliwa kwa Mabavu" ambalo rasimu yake ilipitishwa wiki iliyopita na kamisheni ya UNESCO.

Kufuatia kupitishwa azimio hilo, Quds Mashariki (Jerusalem) Mashariki imesajiliwa rasmi kuwa turathi ya Ulimwengu wa Kiislamu.

Katika kikao cha kamisheni ya UNESCO kilichofanyika tarehe 11 ya mwezi huu wa Oktoba, nchi 24 wanachama ziliunga mkono rasimu hiyo, nchi 26 ziliamua kutopiga kura na nchi sita ambazo ni Marekani, Uingereza, Ujerumani, Uholanzi,Lithuania na Estonia zilipiga kura ya kupinga.

Kwa kupitisha azimio hilo, UNESCO imepinga kuwepo uhusiano wowote wa kidini baina ya msikiti mtukufu wa Al-Aqsa na Mayahudi na kusisitiza kuwa msikiti huo ni mahala patakatifu kwa Waislamu.

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha mwaka huu kwa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni kupitisha azimio dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Mnamo mwezi Aprli, UNESCO lilipitisha azimio la kulaani uchokozi wa Israel na hatua zake haramu dhidi ya uhuru wa Waislamu kutumia msikiti mtukufu wa Al-Aqsa.

Al-Aqsa ni msikiti wa tatu kwa utukufu katika Uislamu baada ya Msikiti mtukufu wa Makka na Msikiti wa Mtume Muhammad SAW wa mjini Madina.

Msikiti wa Al-Aqsa ni msikiti wa tatu mtukufu kwa Waislamu baada ya Msikiti Mtukufu wa Makka na Msikiti wa Bwana Mtume SAW wa Madina.

Kwa miaka kadhaa sasa hatua ya utawala wa Kizayuni ya kuwawekea Waislamu wa Palestina vizuizi na mipaka ya kuingia kwenye msikiti wa Al-Aqsa kwa ajili ya kusali katika eneo la Mashariki la Baitul Muqaddas nafujo na uvamizi unaofanywa na walowezi wa Kizayuni katika eneo hilozimekuwa zikisababisha machafuko na mapigano makali baina ya askari wa Kizayuni na wananchi wa Palestina.

3539048

Kishikizo: iqna unesco quds aqsa
captcha