Kwa mujibu wa gazeti la Japan Times, maonyesho hayo yatakuwa maalumu kwa ajili ya mavazi ya Kiislamu ya Hijabu yanayotumiwa na wanawake Waislamu.
Waandalizi wa maonyesho hayo wanasema sababu kuu ya kuyaandaa ni ongezeko la watalii Waislamu nchini Japan. Mbali na kujitahidi kuimarisha uhusiano wa Japan na nchi za Kiislamu, maonyesho hayo pia yanalenga kuondoa dhana potofu iliyopi kuhusu mavazi ya Kiislamu.
Kwa ujumla kutakuwa na maonyesho manne pamoja na warsha ya miundo ya vazi la Hijabu katika siku hizo mbili.
Maonyesho hayo ya mavazi ya kike ya Kiislamu yatafanyika mjini Tokyo sambamba na maonyesho vya vyakula, bidhaa na huduma Halal.
Zifuatazo ni picha za baadhi ya mitindo ya Hijabu inayotazamiwa kuwasilishwa katika maonyesho hayo.