IQNA

Kongamano la Sekta ya Halal kufanyika Nigeria

22:02 - August 15, 2021
Habari ID: 3474193
TEHRAN (IQNA)- Sekta ya bidhaa na huduma ‘Halal’ duniani ina thamani ya zaidi ya dola trilioni 3 na inawakilisha moja ya sekta zenye mustakabali mwema.

Kwa kuzingatia kuwa idadi ya Waislamu duniani ni zaidi ya bilioni  1.8, sekta hii ina uwezo wa kustawi zaidi.

Mashirika mengi duniani sasa yameazimia kutengeneza bidhaa au kutoa huduma ‘Halal’ kwa mujibu wa mafundisho wa Kiislamu ili kuwahudumia Waislamu na hata wasio kuwa Waislamu wanaotumia huduma hizo.

Nchi za Afrika ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya Waislamu wanaotumia huduma Halal ingawa bado kuna kazi kubwa inayoweza kufwanya kuwafikia Waislamu zaidi.

Kwa mfano nchini Nigeria, Waislamu ni zaidi ya asilimia 50 ya watu wote milioni 100 nchini humo na lakini fursa za soko la Halal bado hazijatumiwa kikamilifu.

Kulingana na Jumba la Biashara na Viwanda la Abuja (ACCI), uamuzi wa kudhamini Maonyesho ya Kimataifa ya Halal kati ya tarehe 14 na 16 Septemba 2021 umechukuliwa ili kuwezesha Waislamu kupata kwa bidhaa na huduma ambazo zimetayarishwa kwa mujibu  na kanuni za Sharia za Kiislamu.

Kwa msingi huo ACCI inaandaa Maonyesho hayo na washirika kutoka Nigeria, Uturuki, India, Malaysia, Indonesia, Misri, Tunisia, Morrocco, UAE, Saudi-Arabia, na nchi zingine za Kundi la D8.

Maonyesho hayo ya Halal Expo Nigeria yatashirikisha kampuni zaidi ya 70 katika biashara anuwai kuanzia chakula na vinywaji, vipodozi, mavazi, fasihi, utalii na hoteli na migahawa.

Maonyesho ya Halal Nigeria 2021 yanalenga pia kuoanisha vyombo vyote vinavyotoa vyeti vya Halal katika taasisi moja inayotambuliwa na serikali.

3990330

Kishikizo: halal nigeria waislamu
captcha