IQNA

Polisi nchini Nigeria washambulia waungaji mkono Sheikh Zakzaky

23:12 - January 26, 2017
Habari ID: 3470815
IQNA- Polisi nchini Nigeria wamewavurumishia mabomu ya kutoa machozi waandamnaji waliokuwa wakimuunga kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo, Sheikh Ibrahim Zakzaky ambaye anaendelea kuwekwa kizuizini kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mamia ya wafuasi wa Sheikh Zakzaky siku ya Alhamisi walifyatuliwa mabomu ya kutoa machozi walipokuwa wakishiriki maandamano ya amani ya kuonyesha uungaji mkono wao kwa kiongozi wao, nje ya bunge la nchi hiyo katika mji mkuu Abuja.

Maafisa wa polisi wa Nigeria walitumia nguvu ziada kuyvunja maandamano hayo ya amani kwa, ambapo watu kadhaa walijeruhiwa. Waandamanaji hao ambao walikuwa wamebeba picha za Sheikh Zakzaky na maberamu yenye ujumbe unaosema, "Muachieni huru Zakzaky" walisikika wakiikosoa vikali serikali ya Nigeria kwa kuendelea kumzuilia Sheikh Zakzaky licha ya agizo la mahakama.

Itakumbukwa kuwa Mahakama Kuu ya Nigeria hivi karibuni ilitoa amri ya kuachiliwa huru Sheikh Zakzaky, lakini serikali ya Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo imepuuza na kukiuka amri hiyo ya mahakama kwa kukataa kumwachilia huru kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu.

Sheikh Ibrahim Zakzaky akiwa na mke wake alitiwa mbaroni na Jeshi la Nigeria mwezi Disemba mwaka 2015 katika kituo cha kidini huko katika mji wa Zaria kaskazini mwa jimbo la Kaduna. Tokea wakati huo Sheikh Zakzaky na mkewe wamekuwa wakizuiliwa katika mojawapo ya vituo vya kijeshi vya nchi hiyo bila kufunguliwa mashktaka.

Jeshi hilo lilidai kuwa wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria walikuwa na njama ya kutaka kumuua Mkuu wa Jeshi la Nigeria, madai ambayo yamekanushwa vikali na wafuasi wa harakati hiyo.

Jeshi hilo katili liliizika miili ya waliouawa katika kaburi moja kwa lengo la kuficha ushahidi wa ukubwa wa jinai hiyo. Inakadiriwa kuwa Waislamu 1000 wasio na hatia waliuawa katika tukio hilo huku Sheikh Zakzaky, ambaye hali yake ya kiafya si nzuri, akiendelea kushikiliwa korokoroni pasina kufunguliwa mashtaka.


3462043
captcha