IQNA

Marekani: Trump aapa kurudisha marufuku ya kusafiri kwa Waislamu wapo atashinda uchaguzi wa 2024

21:44 - October 29, 2023
Habari ID: 3477806
WASHINGTON, DC (IQNA) - Donald Trump aliuambia mkutano wa wafadhili wa Kiyahudi wa Republican siku ya Jumamosi kwamba atarejesha marufuku yake ya wasafiri kutoka nchi nyingi za Waislamu ikiwa atashinda tena urais mnamo 2024.

Trump alisema atawaweka wale aliowataja kuwa eti ni ‘magaidi wa Kiislamu’wenye itikadi kali nje ya Marekani" na "kumtetea rafiki na mshirika wetu, Israel, kwa namna ambayo haijawahi kufanyika­­­­."

Alizungumza kwenye mkutano wa kila mwaka wa Muungano wa Kiyahudi wa Republican huko Las Vegas, Nevada, ambapo alipokea mapokezi mazuri kutoka kwa waliohudhuria.

Trump aliweka marufuku ya kusafiri kwa Iran, Libya, Somalia, Syria, Yemen na, mwanzoni, Iraqi na Sudan mnamo 2017, muda mfupi baada ya kuchukua madaraka. Marufuku hiyo ilikabiliwa na changamoto za kisheria na kutajwa kuwa ni aina ya ubaguzi wa kidini lakini iliidhinishwa na Mahakama ya Juu mwaka wa 2018.

Marufuku hiyo ilibatilishwa na Rais Joe Biden mnamo Januari 2021.

Trump ni miongoni mwa vinara wa chama cha Republican ambao wamejaribu kutafuta kura zaidi kwa kuunga mkono ukatili unaoendelea wa utawala dhalimu wa Israel katika Ukanda wa Gaza, ambapo mashambulizi ya utawala huo tangu Oktoba 7 yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 7,700.

Trump alichukua hatua zaidi na kuvitaja vita vya Israel na Palestina kuwa etini "vita kati ya ustaarabu na ushenzi, kati ya adabu na upotovu, na kati ya wema na uovu," akirejea simulizi ya miongo mingi ya vyombo vya habari vya Magharibi katika kuwadhalilisha watu wa Palestina na kupuuza harakati yao ya kupigania ukombozi wa ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel

Makundi ya kupigania ukombozi wa Palestina yenye makao yake huko Gaza yalifanya Operesheni ya Kimbunga au Tufani ya Al-Aqsa tarehe 7 Oktoba, mashambulizi ya kushtukiza katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, ili kukabiliana na jinai kali za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya watu wa Palestina.

3485780

captcha