IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Kuna haja kulelewa kizazi cha vijana wa Iran wenye imani imara

16:57 - May 03, 2016
Habari ID: 3470287
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitizia wajibu wa kulelewa kizazi cha vijana wa Iran katika msingi wa kuwafanya wajitegemee na wapende kuwa na heshima ya kidini na kusimama imara kupambana na madola ya kibeberu.

Ayatullah Khamenei amesema hayo Jumatatu mjini wakati alipowahutubia maelfu ya walimu kutoka kona zote za Iran na kusisitiza kuwa, suala la kukilea kizazi kijacho cha wananchi wa Iran katika msingi wa kuwa na utambulisho wa kujitegemea, kuchunga heshima na kushikamana na dini ni jukumu hatari la Wizara ya Elimu na Malezi pamoja na walimu nchini.

Amesema, iwapo jamii itakuwa na watu waliopambakia na sifa hizo, bila ya shaka yoyote utaweza kupata maana yake halisi uchumi wa kimuqawama usiotegemea mafuta, sera za utamaduni huru, siasa za kigezo kizuri cha matumizi na moyo ya kusimama kidete na kutotetereka mbele ya mabeberu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, Marekani na mabepari wa Kizayuni pamoja na madola mengine ya kiistikbari ni dhihirisho la mfumo wa kibeberu duniani na kusisitiza kuwa, mfumo wa kibeberu unataka vizazi vijavyo vya mataifa ya dunia viwe na fikra, utamaduni, mitazamo na misimamo inayokubaliana na madola ya kibeberu na hatimaye watu wenye vipawa, wanasiasa na watu wenye taathira katika jamii za nchi hizo watende kila wanachonyweshwa na madola ya kibeberu.

Ayatullah Khamenei amesema, wanafikra wa nchi za Magharibi wamekuwa wakisisitiza mara chungu nzima kuwa, badala ya kutumia mbinu ya karne ya 19 ya kuzivamia na kuzikoloni nchi nyingine, njia bora kabisa na yenye gharama ndogo zaidi ni kujipenyeza na kupandikiza fikra za kikoloni kati ya vijana wa nchi hizo na kulea watu wenye vipaji katika jamii ambao kimsingi watakuwa ni maafisa wa kijeshi wa kulinda na kupigania malengo ya mabeberu.

Amesema, baadhi ya tawala za eneo hili hivi sasa ni mfano wa wazi wa matunda ya mipango hiyo ya muda mrefu ya madola ya kibeberu kwani tawala za nchi hizo zinafanya kila jambo ambalo linatakiwa na Marekani na wako tayari kuyaletea madhara mataifa yao kwa ajili ya kuwaridhisha Wamarekani.

3494124


captcha