IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Wasomi wa kidini washiriki kikamilifu katika jamii, nchi

0:13 - May 15, 2016
Habari ID: 3470313
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa wito kwa wasomi wa kidini kushiriki kilamilifu katika mambo yote yanayohusu nchi na jamii

Aidha, Kiongozi Maudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametaja mambo matatu muhimu ambayo ndiyo majukumu makuu ya watu wa dini. Ameyataja mambo hayo kuwa ni kuwaongoza watu kifikra na kidini, kuwaongoza watu kisiasa na kuwafanya kuwa na muono wa mbali na kuwaongoza watu na kushiriki kivitendo katika kutoa huduma za kijamii. Ayatullah Ali Khamenei amesema hayo Jumamosi asubuhi mjini Tehran mbele ya wakuu, walimu na wanafunzi wa Hawza (vyuo vikuu vya kidini) za mkoa wa Tehran na kusisitiza kuwa: Wanafunzi wa kidini wanapaswa kujiidilisha kupata elimu inayotakiwa na ustahiki wa kuwa wanafunzi wa dini, ili waweze kutekeleza vizuri majukumu yao katika jamii na katika dunia hii tofauti ya leo. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewausia pia wanafunzi wa dini kujua thamani ya kuwa wanafunzi wa kidini na kusisitiza kwamba: Lau kama katika jamii kutakuwa na utaalamu wa kila namna, lakini jamii hiyo ikakosa kuwa ya kidini, basi taifa la jamii hiyo litapata hasara duniani na Akhera na kwamba ni jukumu adhimu la maulamaa, wanavyuoni na wanafunzi wa dini kuibadilisha jamii kuwa jamii ya kidini. Amesema, Uislamu usioona mbali, wa kitaasubu, usio na welewe sahihi kuhusu uhakika wa mambo ya kimaanawi na wenye fikra mgando, ni mfano wa wazi wa fikra potofu. Pia amesema, Uislamu mwingine unaopambana na Uislamu wa kweli ni ule Uislamu wa kuokota na Uislamu wa Kimarekani ambao unafanya kila njia kukabiliana na Uislamu wa kweli. Vile amewahimiza maulamaa na watu wa dini kuwaongoza watu kisiasa, kidini na kivitendo katika masuala yote ya nchi na jamii.

3497842

captcha