IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Kutoamini mabeberu, hasa Marekani, ni nukta ya nguvu laini za Iran

0:16 - September 19, 2016
Habari ID: 3470570
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema miongoni wa nukta muhimu za nguvu laini za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kutoyaamini hata kidogo madola ya kibeberu, hasa Marekani.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo Jumapili mjini Tehran katika mkutano na washiriki wa kongamano la kitaifa la makamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa, kutokuwa na Imani na madola hayo ya kibeberu yakiongozwa na Marekani kunapasa kuongezeke zaidi siku baada ya siku.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi amesema kutokuwa na imani hata chembe na Marekani ni matokeo ya utumiaji akili ambao umetokana na fikra, mtazamo wa kina na tajiriba; na akafafanua kwa kusema: "Suala la uadui wa Marekani limeshuhudiwa katika kipindi cha miaka mingi baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran,katika kadhia za karibuni za mazungumzo ya nyuklia na katika masuala mengine; na kufanya mazungumzo na Marekani sio tu hakuna faida bali kuna madhara pia".

Kwingineko katika hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGS) ni "ngome imara ya Mapinduzi" na "chombo muhimu cha kulinda usalama wa ndani na nje".

Ameongeza kuwa: "Kudumisha, maana yake si kukomea katika wakati mmoja, bali sambamba na kubadilika zana na hatua anazopiga adui, IRGC nayoinatakiwa isitoshekena hatua ilizopigakatika uga wa sayansi,teknolojiana ugunduzi mpyabali ipigehatua mbele zaidi."

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi amesema"usalama" ni maudhui muhimu sana na ni utangulizi wa maendeleo ya kimaanawi na kimaada ya jamii na akaongezea kwa kusema: "Miongoni mwa majukumu ya IRGC ni kudhamini usalama wa ndani na nje; na endapo hakutakuwepo na usalama wa nje kwa kutochukua hatua za kuzuia uchokozi wa adui nje ya mipaka, usalama wa ndani pia utatoweka".

3531220

captcha