IQNA

Ghadhabu za Wazayuni baada ya UNESCO kutangaza Al Aqsa ni milki ya Waislamu

22:54 - October 14, 2016
Habari ID: 3470611
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO limepitisha azimio na kusema Msikiti wa Al Aqsa ni milki ya Waislamu kwamba Mayahudi hawana haki katika msikiti huo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, siku ya Alhamisi UNESCO ilipasisha azimio ambalo lilikosoa vikali sera za utawala wa Kizayuni wa Israel katika Msikiti wa Al Aqsa ulio katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo. Azimio la UNESCO limepinga madai yoyote ya Wazayuni kuwa msikiti huo una uhusiano na Mayahudi.

Azimio hilo aidha limelaani Israel kwa kuwazuia Waislamu kuingia katika msikiti huo. Azimio hilo ambalo limeitaja Israel kama ‘dola ghasibu’ limelaani pia hatua ya askari wa Israel kuuhujumu Msikiti wa Al Aqsa mara kwa mara.

Azimio halikadhalika limesisitiza kuwa mji wa Quds ni mtukufu kwa dini tatu za Uislamu, Ukristo na Uyahudi sambamba na kipengee maalumu kuhusu Msikiti wa Al Aqsa ambacho kinasema msikiti huo ni eneo takatifu la Waislamu pekee. Katika upigaji kura kuhusi azimio hilo, nchi 26 zimejizuia kupiga kura, huku 24 zikiunga mkono azimio hilo na sita zikipinga.

Hakuna nchi yoyote ya Ulaya iliyounga mkono azimio hilo ambalo limewakasirisha wakuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel ambao wametangaza kukata uhusiano wao na UNESCO. Azimio hilo liliwasilishwa na Algeria, Misri, Lebanon, Morocco, Oman, Qatar, Sudan na kuungwa mkono na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mwezi Agosti ilibainika kuwa, taasisi za utawala wa Kizayuni wa Israel zinafanya maandalizi ya kuanza kutekeleza mradi wa ubomoaji wa msikiti wa Al-Aqsa na kujenga mahala pake maabadi iitwayo "Hekalu la Tatu la Sulaiman".

Kikinukuu kanali za televisheni za Israel, kituo cha habari na kimataifa cha Mashariki ya Kati cha Palestina kimetoa ripoti maalumu na kutangaza kuwa taasisi za Israel zinasubiri maamuzi ya kisiasa ya Tel Aviv ili kuanza kutekeleza mradi huo.

Shirika la habari la Palestina la Al-Ra'y liliripoti kuwa taasisi hizo za Israel zinajiandaa kupeleka vifaa vya ubomoaji huko Baitul Muqaddas kwa ajili ya kuubomoa msikiti wa Al-Aqsa na Qubbat Al-Sakhra na kujenga 'hekalu la tatu'.

Msikiti wa Al-Aqsa ni msikiti wa tatu mtukufu kwa Waislamu baada ya Msikiti Mtukufu wa Makka na Msikiti wa Bwana Mtume SAW wa Madina.

Kwa miaka kadhaa sasa hatua ya utawala wa Kizayuniya kuwawekea Waislamu wa Palestina vizuizi na mipaka ya kuingia kwenye msikiti wa Al-Aqsa kwa ajili ya kusali katika eneo la Mashariki la Baitul Muqaddas nafujo na uvamizi unaofanywa na walowezi wa Kizayuni katika eneo hilozimekuwa zikisababisha machafuko na mapigano makali baina ya askari wa Kizayuni na wananchi wa Palestina.

3537564

captcha