IQNA

Sayyid Nasrullah:

Siku ya Quds ni siku ya kuung'oa utawala bandia wa Israel

19:04 - July 02, 2016
Habari ID: 3470427
Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa lengo la kutangazwa Siku ya Kimataifa ya Quds ni kubakisha hai kumbukumbu ya Quds tukufu na kuwafanya Waislamu wasisahau eneo na msikiti huo mtakatifu.

Sayyid Hassan Nasrullah ambaye alikuwa akihutubia umati mkubwa kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds mjini Beiruti amesema Siku ya Kimataifa ya Quds ni siku ya kuandika historia na kuung'oa utawala bandia wa Israel. Ameongeza kuwa hayati Imam Khomeini aliitangaza Ijumaa ya mwisho ya kila mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds ili kadhia ya mapambano ya Wapalestina ibakie hai daima na isisahaulike. Amesisitiza kuwa, ardhi ya Palestina kuanzia Bahari ya Mediterania hadi mto wa Jordan inakaliwa kwa mabavu na kwamba kupita kwa miaka hakuipi Israel haki na uhalali wa kuikalia ardhi hiyo kwa mabavu.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema utawala ghasibu wa Israel unapaswa kuangamizwa na watu wa Palestina warejeshewe haki yao.

Sayyid Nasrullah amepinga aina yoyote ya mapatano na utawala haramu wa Israel na kusema: Njia pekee mbele ya Wapalestina na mataifa mengine ya Mashariki ya Kati ni kupambana na kusimama kidete dhidi ya utawala huo bandia.

3511879


Vilevile amezikosoa baadhi ya nchi za Kiarabu zilizoutambua rasmi utawala haramu wa Israel na kusema jambo hilo halikubaliki.

Katibu Mkuu wa Hizbullah pia amesema vibaraka wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Isarel katika nchi kama Syria, Yemen, Bahrain na Libya wanaendeleza vita na mapigano na wanazuia jitihada za kupatikana suluhisho la kisiasa katika nchi hizo.

Sayyid Hassan Nasrullah amesema mahudhurio ya magaidi katika mkutano uliofanyika hivi karibuni katika mji wa Herzliya huko Israel ni ushaidi wa nafasi ya Israel katika kudumisha vita nchini Syria.

Vilevile amelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyowalenga Wakristo kusini mwa Lebanon na yale yaliyotokea katika uwanja wa ndege wa Ataturk mjini Istanbul huko Uturuki.

captcha