IQNA

Waziri wa Ulinzi wa Iran

Wamagharibi hawana nia ya kupamana na ugaidi

14:24 - December 29, 2016
Habari ID: 3470765
IQNA: Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema muungano wa Wamagharibi wa kupambana na ugaidi katika eneo la Mashariki ya Kati ni hatua ya kimaonesho na ya hadaa.

Brigedia Jenerali Hussein Dehqan, Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo katika mahojiano maalumu na kanali ya televisheni ya Russia Today na kueleza bayana kwamba Wamagharibi hawana nia ya dhati ya kupambana na ugaidi katika nchi za Iraq na Syria. Ameongeza kuwa, kile ambacho kina umuhimu wa kwanza kwa eneo hivi sasa ni kurejesha amani na uthabiti na kutokomeza ugaidi pasina kufuata tafsiri za kindumakuwili za Magharibi kuhusu ugaidi na magaidi.

Brigedia Jenerali Dehqan amebainisha nukta hiyo kwa uwazi kabisa na kueleza kwamba Daesh na Fat-hu Sham (Jabhatun-Nusrah) hayawezi kushirikishwa katika usitishaji vita nchini Syria na akasisitiza kwa kusema, katika kampeni ya kupambana na ugaidi, pande zote zinapaswa ziheshimu na kutekeleza uamuzi wa kukomesha utoaji misaada na uungaji mkono wa kisiasa, kifedha na kijeshi kwa magaidi.

Vilevile amesema majeshi ya Uturuki yanalazimika kuondoka katika ardhi ya Syria iwapo Damascus inataka kutimizwa takwa hilo.

Brigedia Jenerali Hussein Dehqan amesema kuwa, Iran inalitambua suala la usalama wa Mashariki ya Kati kuwa ndio usalama wa taifa hili na inaamini kuwa, ukosefu wa amani na uwepo wa machafuko katika eneo hili ni jambo linalohatarisha usalama na amani ya dunia nzima.

3557309

captcha